TAMKO RASMI CHADEMA UK
CHADEMA UK awali ya yote tunapenda kutoa pole kwa waTanzania na wapenzi wa CHADEMA waliopatwa na kukutwa na janga la kurushwa kwa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA wa kuhitimisha shughuli za kampeni za uchaguzi wa madiwani huko Arusha. Tunatuma salam zetu kuwafariji wale wote walioguswa kwa namna moja ama nyingine katika jambo hili.
Kama waTanzania, tunapinga vikali na kukemea kitendo hichi kwa nguvu zetu zote. Mazingira na jinsi kitendo hichi kilivyotekelezwa tuna kila sababu ya kuamini kwamba hili ni tendo la kigaidi. Na kwa sababu hiyo ni jukumu la mamlaka (yaani serikali) na vyombo vyake vya dola kulinda na kuepusha matendo ya kigaidi kama haya.