Tuesday, May 28, 2013

Mkutano wa CHADEMA UK na Mjadala wa waTanzania

Napenda kukumbusha kuhusu mjadala mkubwa na wa kihistoria wa waTanzania utakaofanyika 3Sixty, University of Reading siku ya tarehe 01/06/2013.


Kwa taarifa tu, kutakuwa na usafiri kwa wale watakaohitaji. Usafiri wa basi utaanzia London saa 4:00 (nne kamili) asubuhi. Kama unahitaji huduma hii unashauriwa kuwasiliana na Bernad Irondo kwenye namba hii: 07804804963 kabla ya siku ya Jumatano tarehe 28/05/2013.

Kwa hisani ya Funguka Forums, mjadala utakuwa unachukua maswali live kupitia Tweeter (@fungukaforums). Pia updates za mjadala zitakuwa zinarushwa live kwenye www.fungukaforums.com , facebook (www.facebook.com/funguka.fungukaforums). Pamoja na facebook, mjadala utaruhusu ushiriki kwa kupitia Skype (funguka). Hii ni kuwapa nafasi ya kushiriki wale wote wakakaoshindwa kuhudhuria siku hiyo kutokana na sababu mbalimbali. Haijalishi mahali ulipo, shiriki kwa kupitia Tweeter au Skype ama fuatilia kwenye forum au facebook. Hata hivyo kama hutahudhuria ila una mchango wako unaogusa moja ya topic zitakazozungumzwa siku hiyo tafadhali tuma swali/maoni kwenye email: team@fungukaforums.com. Maswali yote yatakusanywa na kusoma wakati mjadala ukiendelea.

Karibuni wote na umkaribishe/mjulishe mwenzako.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...