Saturday, September 28, 2013

End of the Year BBQ Party in Reading!


CHADEMA UK inawakaribisha waTanzania na wapenzi wote wa CHADEMA kwenye barbeque (End of the Year BBQ) party itakayofanyika Comunity Hall/Back Garden, 44 Watlington street, RG1 4RJ Reading tarehe 05-10-2013.

Mgeni rasmi atakuwa ni mwanasiasa mwenye kipaji cha pekee na muhimili muhimu wa CHADEMA – katibu wa CHADEMA Arusha na kanda ya kaskazini ndugu Amani Golugwa.

Itakuwa ni siku nzuri kujiburudisha kwa nyama choma, vinywaji na muziki free of charge. Lengo ni kuwakutanisha wapenda maendeleo katika kubadilishana mawazo na kujumuika katika harakati za kimaendeleo kwa taifa.

Hii shughuli si kwa wanaCHADEMA peke yake. Kila mTanzania mpenda maendeleo anakaribishwa kuhudhuria. Ni wakati mzuri kukaa pamoja tukijiburudisha huku tukibadilishana mawazo on party lines kiutu uzima bila malumbano. Wakati ni huu kuonesha utashi na ukomavu wa kisiasa.

Chakula na vinywaji bure!!!

Karibuni wote

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...