Tuesday, May 21, 2013

Mjadala wa waTanzania UK Kufanyika University of Reading

Siku ya Jumamosi tarehe 01/06/2013, waTanzania waishio UK watakutana kwa ajili ya mjadala mkubwa utakaohusu mwaswala yafuatayo: Elimu; Katiba; Muungano; na Utaifa. Mjadala utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa University of Reading. Hii ni nafasi ya kipekee kwa waTanzania kuzungumzia mambo muhimu yanayoihusu jamii yetu bila kujali itikadi, imani, rangi au kitu kingine chochote. Vikundi mbali mbali vya kidini, kisiasa na kijamii vitakuwepo.

Japokuwa mjadala unafanyikia UK, waTanzania wote wenye nia ya kushiriki kutoka mahali popote pale duniani wanaweza na wanakaribishwa kushiriki. Kama ungependa kushiriki kutoka sehemu yoyote ulipo, unaweza kufanya hivyo kwa kupitia tweeter account itakayotolewa hivi karibuni.

Mjadala utarushwa kwenye YouTube channel. Pia kwa hisani ya Funguka Forums mjadala utakuwa unarushwa live kwenye fungukaforums.com. Pia updates zitakuwa zikitolewa kwa kupitia facebook na twitter.

Karibuni wote tushiriki kwa mapenzi ya nchi yetu.

"Usiulize Tanzania imekufanyia nini. Jiulize wewe umeifanyia nini nchi yako."

G Mboya

Secretary

CHADEMA UK

(+44)(0)7846783365 (m)

secretary@chademauk.org.uk

www.chademauk.org.uk

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...