Monday, June 3, 2013

Mjadala wa WaTanzania UK Wafana

Kamati iliyoandaa mjadala wa waTanzania uliofanyika Reading University siku ya Jumamosi tarehe 01-06-2013 inapenda kuwashukuru sana waTanzania wote waliohudhuria. Mjadala ulikuwa wa mafanikio ulioleta changamoto ya pekee kwa watu wengi sana. Japokuwa washiriki walitoka kwenye vyama mbali mbali, dini tofauti tofauti, makabila tofauti, elimu tofauti, n.k., wakati wa mjadala kilichotawala na kuonekana dhahiri ni uTanzania. WaTanzania walionesha mshikamano wa hali ya juu kwa kuchambua topics kwa kuheshimiana na kwa weledi mzuri. Wachangiaji walionesha uelewa mkubwa katika mambo mengi sana.
Mjadala huu ulipokewa vizuri na kukubalika kwa wengi walioshiriki. Imeonekana dhahiri kwamba waTanzania wana hamu na chachu ya kujikomboa kutoka kwenye umaskini. Tatizo lililopo ni ukosefu wa platform mbali kabisa na serikali inayounganisha nguvu ya watu ili kwa pamoja wapiganie haki zao. WaTanzania wana kiu ya maendeleo. Japokuwa baadhi wamewabeza na kusema waTanzania ni wavivu ndiyo maana ni maskini, dhana hii argument nyepesi isiyoangalia na ku-undermine juhudi za mTanzania wa kawaida ambaye usiku na mchana anahangaika kutafuta kujitosheleza. Wanaomlaumu mTanzania wa kawaida hawayajui hayo na wameziba masikio yao. Kwa hivyo wana Diasporas wamelitambua hilo na wameamua kuchukua hatua ili wahakikishe sauti zao zinasikilizwa.

Kwa sababu hiyo washiriki waliafikiana kwa nguvu moja kufanya yafuatayo:
1.    Kuiendeleza na kuikuza platform hii ya mjadala itakayokuwa ikifanyika mara kwa mara.
2.    Kuunganisha nguvu za waTanzania ili kufanya ili kupigania maendeleo yetu
3.    Kuelimisha jamii ili kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii yetu

Hivyo tunapenda kuwashukuru wote walioandaa shughuli hii pamoja na washiriki wote. Shukrani ya pekee kwa waTanzania kutoka sehemu mbali mbali dunaini walioshiriki kupitia twitter, facebook na email. Bila kuwasahau wadhamini wetu: www.fungukaforums.com kwa kazi kubwa.

Mambo mawili for certain:
1. SAUTI YAKO HAITAENDA BURE
2. KWA PAMOJA NA KWA NGUVU ZETU TUTAWEZA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...